
Picha ya Irene Uwoya na Msami Baby
Msami Baby anasema upendo na kumsaidia mtu sio lazima muwe kwenye mahusiano na Irene Uwoya alimsaidia baada ya kupata ajali ya gari na kumalizana ishu za polisi.
"Mimi nayeye ni washkaji tu, nakumbuka kuna siku nilipata ajali ya gari usiku, asubuhi nikawa polisi hivyo nikawa sipo vizuri mfukoni kwa haraka haraka nikampigia simu Irene Uwoya akanitumia laki 5"
Msami ameongeza kusema wakati anapata msaada huo kutoka kwa Irene Uwoya tayari walikuwa washaachana na hawakuwa tena kwenye mahusiano.