Jumatano , 7th Jul , 2021

Huduma za ku-stream muziki ndio chanzo kikubwa cha mapato kwa wanamuziki ulimwenguni kote ambapo katika kipindi cha mwaka 2019, ku-stream muziki pekee kulitengeneza zaidi ya dola Bilioni 11.1, na kufanya tasnia ya muziki kuwa na mabadiliko makubwa.

YouTube

Hizi ndizo Platforms  zinazolipa vizuri zaidi  

Napster – Ndio jukwaa linaloongoza orodha kwa malipo makubwa ambapo hulipa dola 0.00916 kwa kila mkondo (per-stream), ambapo msanii anaweza lipwa hadi dola 9,160 kwa mibofyo (clicks) Milioni 1 ambazo ni sawa na Ths. Milioni 21.24.

Apple Music – Hulipa dola 0.00675 kama mapato kwa kila wimbo unapochezwa, ambayo inamaanisha kuwa wasikilizaji milioni 1 wataingiza dola 6,750 kwa msanii, sawa na Ths Milioni 15.7.

Deezer – Inachukua nafasi ya tatu kwa mapato ambapo msanii anaweza kupata dola 0.00562 kwa kila hit, ambayo ni sawa na dola 5,620 kwa streams milioni 1 na kwa Ths ni Milioni 13.03

Sasa kwa wasanii wanaotumia Deezer watalazimika kupata mibofyo (clicks) 224 ili kupata dola 1,260 sawa na Ths Milioni 2.9.

Amazon Music – Wao hulipa dola 0.00426 kila wimbo unapochezwa/kusikilizwa na msanii anaweza pata dola 4,260 kwa wasikilizaji milioni 1 ambazo ni sawa na Ths Milioni 10.

Spotify –  Huduma hii maarufu ya ku-stream muziki hulipa wasanii dola 0.00348 kwa hit, au dola 3,480 ambazo ni sawa na Ths  8.07 kwa wasikilizaji milioni 1. 

Watumiaji wa Spotify watalazimika kupata angalau Clicks 362 ili akaunti zao za benki kupata dola 1,260 ambazo ni sawa na Ths Milioni 29.2. 

Pandora – Ni mmoja ya mtandao wa zamani kabisa kwenye soko, hutoa karibu dola 0.00203 kama mapato kwa kila wimbo unapochezwa/sikilizwa na dola 2,030 ambazo ni sawa na Ths 6 kwa wasikilizaji milioni 1. 

YouTube  –  Jukwaa maarufu la ku-stream muziki duniani kote ambalo linalipa kidogo kwa watumiaji ambapo 0.00154 kwa kila unapochzwa/kusikilizwa (views) na dola 1,540 ambazo ni swa na Ths Milioni 4 wa kila views milioni 1. 

Userbase ni kitu cha pili muhimu zaidi wakati wa kuzingatia mapato, kwa hivyo ni muhimu kuzingatia jambo hili kabla ya kuruka kwenye jukwaa fulani.