
Picha ya Rayvanny kulia, kushoto ni Producer Zest
Kupitia Instagram yake Producer Zest amepost video ya zamani ya Rayvanny ambayo anadai alimsaidia ku-shoot video na kurekodi audio kwa kuandika.
"Sio kwamba namchukia uyu dogo, nimemsupport sana toka akiwa underground nyumbani Mbeya mpaka amekuwa star huwa namsupport bila malipo yoyote lakini mwisho wa siku anakulipa dharau".
"Acheni niwaambie ukweli dogo anamalizana vibaya sana na watu waliomsupport toka zamani sio mimi tu hata Gachi B alimalizana naye vibaya. Ni kweli unatakiwa kutenda wema na kwenda zako ila ni vyema kuongea ukweli ili kuwajenga na wengine".