Jumanne , 6th Nov , 2018

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro, Joseph Haule au Prof. Jay, amewapiga marufuku wasanii wenzake wanaomfuata kuomba msaada pindi wanapokuwa na nyimbo zao.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Prof. Jay ameandika ujumbe wa kuwataka wasanii wote wasiompa suport kutomfuata na kumuomba suport pale wanapotoa kazi mpya kwakuwa wao hawampi sapoti kwenye kazi zake.

“Hii ni kwa wasanii wenzangu wote ambao kila nikitoa kazi zangu wanauchuna kama hawanioni na hawataki Kunisupport ila wao kila siku wapo kwenye inbox yangu wakiomba niwapost na ninafanya hivyo mara kwa mara, kuanzia sasa hivi msije tena inbox kwangu”, ameandika Prof. Jay.

Hivi karibuni Prof. Jay ameachia kazi mpya inayokwenda kwa jina la 'Yatapita', ambayo ameilalamika kupata ushirikiano mdogo kutoka kwa wasanii wenzake wa hapa bongo.