Rais Magufuli atoa neno kwa wanaozurura

Jumatano , 20th Nov , 2019

Rais wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli amesema ametoa kibali kwa wafanyabiashara wadogo, wafanye biashara zao mahali popote na si kwa ajili wapiga debe kuzulura.

Rais wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli .

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa ziarani mkoani Morogoro wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Msamvu ambao walijitokeza barabarani kwa ajili ya kumueleza matatizo yao mbalimbali.

Rais Magufuli amesema kuwa "wale wengine wanaofanya biashara ndogondogo nilishasema wasionewe ndiyo maana nilitoa vitambulisho na nilisema mfanye biashara mahali popote lakini sikusema wapiga debe na wazururaji waendelee kuzurula tu, kuna sheria na mimi nimeapa kulina sheria"

Kwa sasa Rais Magufuli yuko mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi