
Mkali wa RnB Rama Dee
Rama Dee amesema licha ya kukaa ndani kwa muda wote huo, analipwa kama kawaida na kuna baadhi ya kazi za kiofisi anazifanya akiwa nyumbani, lakini anashangaa kuona kuna baadhi ya wasanii wanaachia kazi nzuri lakini bado wanamuomba pesa.
Akieleza hayo kupitia show ya Dadaz ya East Africa Tv, Rama Dee amesema muziki wa Bongo ni local sana na yeye binafsi ameacha kuimba miaka miwili iliyopita.
"Mziki wa Tanzania upo local sana, sasa hivi nimefanya mapumziko ya kufanya muziki kwa miaka miwili, kati ya hii miaka miwili niliyopumzika nimeona wasanii wengi kazi zao zimefanya vizuri lakini nikikuonyesha meseji utaona wanavyonipiga vizinga" amesema Rama Dee.