Jumatatu , 20th Dec , 2021

Kupitia Instagram ya rafiki wa karibu na Lulu Diva, Wema Sepetu ameshea ratiba kamili kuhusu ulipo msiba wa mama Lulu Diva pamoja na mazishi yake yatakapofanyika.

Picha ya Lulu Diva na mama yake mzazi enzi za uhai wake

"Mwili utapita nyumbani kwa Lulu Diva, Mbezi Beach kwa Mwamunyange mbele ya kota za police mpya, saa 7 mpaka 9 mchana kwa ajili ya dua".

"Baada ya Dua tutaanza safari ya kuelekea Tanga - Muheza- Mafele ifikapo saa 10 jioni, na mazishi yatafanyika kesho saa saba mchana huko huko Tanga- Mafele wilaya ya Muheza".