Jumatatu , 2nd Sep , 2019

Muigizaji Mkongwe wa Bongo Movie Vincent Kigosi 'Ray', amenyoosha maelezo kuhusu watoto ambao anataka kuwa nao katika familia pamoja na kutumia ukongwe wake katika kazi zake.

Vincent Kigosi 'Ray'

Ray ameieleza hayo EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuhusu kukaa kimya kwa muda mrefu.

"Mimi ni mkongwe mtu wa zamani, hata mambo yangu nitayachanganya kizamani na kisasa ili nipate kitu kikubwa katika soko la filamu la Tanzania, sijaonekana siku nyingi lakini nakuja sasa, sisi ni watu wazima tunaangaliaga tulikosea wapi na tunatakiwa kuelekea wapi".

Aidha ameendelea kueleza kuwa ana kitu kikubwa anakifanya kinakuja kuanzia mwezi Oktoba mwanzoni au mwishoni ambapo ataangalia ratiba yake itakavyokuwa kabla ya mwaka huu haijaisha.

Pia ameeleza kuhusu mpango wa kuongeza watoto wengine ambapo amesema kila kitu ni mipango ya Mungu, hata mtoto wao hawakupanga kuzaa ila imetokea ikawa hivyo, ila anategemea kupata watoto wawili tu anafunga kazi.

Hata hivyo Ray amesema ana mpango wa kuachia filamu itakayohusu maisha yake na familia kuanzia mtoto wake na mama wa mtoto huyo Chuchu Hansy.