Rihanna na Drake tena!!

Jumamosi , 7th Sep , 2019

Ni takribani miaka mitatu imepita tangu tuipate Albamu ya Rihanna ya mwisho kutoka ilikuwa ni 'Anti' iliyokuwa na singo kali kama Work, Kiss It Better, Needed Me, Love On The Brain na nyingine nyingi.

Rihanna na Drake

Sasa huenda kabla mwaka huu haujaisha tunaweza kupata Albamu mpya. kutoka kwake mwezi ukitajwa ni Disemba katika tarehe za mwanzo inaweza ikaachiwa.

Hayo yametajwa na mkuu wa lebo ya Universal Music Group (UMG) nchini Ufaransa, Olivier Nusse katika ufunguzi wa tamasha la Open Session, lililofanyika Ijumaa ya tarehe 06 ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo likisimamiwa na UMG.

Olivier alitaja orodha ya albamu ambazo zitaachiwa na Lebo hiyo kabla ya mwaka huu kuisha huku majina ya Rihanna na Drake  yakiwemo ndani.

Mwanzoni mwa mwaka huu Rihanna katika moja ya mahojiano alisema juu ya ujio wa albamu ambayo anatamani kuiachia lakini kuna vitu anaona havijakaa vizuri sababu anataka kuleta kitu cha utofauti.

"Sioni sababu ya kuileta haraka lakini nataka itoke, kwa ambapo nimefikia naona ni pazuri lakini kwa sasa jinsi nilivyo hata kama nitakosa muda wa kushuti video nitaachia albamu kwanza," aliongea.

Wasanii wengine wakali ukimtoa Rihanna na Drake ambao albamu zao zinatarajiwa kuachiwa mwaka huu kabla hujaisha ni Kanye West, Migos na The Weeknd.