Ijumaa , 7th Mar , 2014

Msanii mkongwe wa michano kutoka Kenya, Roba kutoka Kleptomaniax, kundi lililowahi kutikisa chati mbalimbali za muziki Afrika Mashariki miaka ya nyuma, ametangaza ujio wake mpya ambapo anatarajia kutua Jijini Nairobi hivi

Roba ambaye aliamua kugeukia shughuli nyingine za kifamilia pamoja na biashara huko Pwani ya Kenya Malindi, amesema kuwa muziki hauwezi kuiacha damu yake, na sasa ambapo mambo yake ya biashara na familia yamekaa juu ya mstari, ameona kuwa ni muda muafaka wa kurudi katika gemu.

Msanii huyu alitoweka katika ramani ya muziki mara baada ya kundi la Kleptomaniax kusambaratika na kila msanii kuanza kushughulika na kazi zake binafsi, na taarifa za ujio wake mpya tayari zimeibua chachu na hamu mpya ya kusikia ladha atakayorejea nayo.