
Picha ya MwanaHipHop Roma Mkatoliki
Kupitia maelezo ambayo ameyaweka kwenye mtandao wa Twitter, Roma Mkatoliki ameandika anapata changamoto pale anapomkuta kijana kwenye sekta hiyo kwa sababu kuna wengine wanafanya makusudi kwenye vipimo.
"Zama hizi ukienda kwenye ofisi, taasisi, kampuni, mashirika na idara nyingi wengi wa watumishi utakaowakuta ni vijana, ni jambo zuri ila napata changamoto sana ninapompeleka mke wangu kliniki na kumkuta daktari anayemfanyia vipimo ni yanki tupo sawa au pengine nimemzidi umri" ameandika Roma.
Aidha Roma ameendelea kuandika "Halafu ndiyo anampima mke wangu njia ya uzazi, mara ampapase papase tumbo, tena kuna wengine wana makusudi utasikia samahani naomba subiri hapo nje kwenye benchi, sawa ni taaluma yake na inapaswa kumuamini ila mimi napataga wakati mgumu sana".