
Msanii wa muziki nchini Saraha
Saraha ameongea na eNewz kuwa amefurahi kuwa mashabiki wanazikubali sana kazi zake nchini na kuelezea kuwa atarudi nyumbani Sweden kwa ajili ya kuendelea kusambaza muziki wake.
Aidha, mwanadada huyo ameongezea kuwa amekwisha fanya mipango ya kufanya kazi pamoja
na wasanii nchini Sweden ambao pia wanafanya muziki wa kiafrika zaidi.
Kwa sasa dashosti huyo amerelease albam yake mpya aliyoibatiza jina 'Mbele Kiza' inayotamba Ulaya ambayo inaendelea kupata soko kubwa kupitia mitandao ya kijamii.
