Tangazo hilo linakuja ikiwa ni muda mfupi tangu aachie miradi yake miwili ya mwaka 2024, ikiwemo album ya We Don't Trust You aliyoshirikiana na mtayarishaji maarufu Metro Boomin, iliyotoka rasmi tarehe 22 Machi 2024. Album hiyo ilifanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki na kupokelewa kwa hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki.
Baadaye, wawili hao walifuata na mwendelezo wa mradi huo kupitia album ya We Still Don't Trust You, iliyotoka tarehe 12 Aprili 2024, ikiwa na nyimbo zaidi na mitindo tofauti iliyoonyesha ubunifu wa hali ya juu.
Hadi sasa, Future hajaweka wazi jina la album hiyo mpya wala tarehe rasmi ya kuachiwa kwake, lakini mashabiki wengi tayari wana matarajio makubwa kufuatia mafanikio ya kazi zake za hivi karibuni.




