Jumatatu , 20th Jul , 2015

Diva wa miondoko ya Bongofleva Shantiver amesema yeye ni mmoja wa wasanii ambaye kwa sasa yupo mstari wa mbele kuwahamasisha vijana wenzake kujiandikisha na kupiga kura kwa ajili ya kumchagua kiongozi bora atakayeiongoza nchi

msanii wa miondoko ya bongofleva Shantiver

Shantiver ameongea na eNewz kuhusiana na wajibu wa kijana kutambua kuwa kura yako ina thamani kubwa na pia ameifagilia kampeni hiyo ya ZamuYako2015 ya EATV ambayo hakika vijana wataendelea kuhamasishwa kupiga kura.