Jumanne , 28th Jul , 2015

Diva wa miondoko ya Bongofleva nchini Shantiver ambaye anatamba na wimbo wake alioshirikiana na msanii CBH uliobatizwa jina 'Leo' amesema kuwa ukimya alionao hivi sasa ni kutokana na changamoto za kidunia na si kuwa gemu imemshinda.

Diva wa miondoko ya Bongofleva nchini Shantiver

Shantiver ameiambia eNewz kuwa kutokana na ukimya huo yeye binafsi bado amejipanga kutoa kazi zake ndani ya mwezi huu, huku akiwasihi mashabiki kuwa yupo fiti na ukweli wote wataupata kupitia singo yake inayotarajiwa kutambulishwa hivi karibuni.