Jumanne , 18th Aug , 2020

Msanii mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa Shilole amefunguka kuwa msanii Baba Levo amekuwa akishika simu yake mara kwa mara kumchunguza kama amepata mwanaume mwingine.

Picha ya pamoja ya wasanii Shilole na Baba Levo

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital amesema, Baba Levo simu yake huwa haina bundle,  hivyo hutumia ya kwake ambapo akishaichukua anakuaga ujumbe wa kawaida na ujumbe wa Instagram "DM" ili kujua kama amepata mwanaume mwingine anayewasiliana naye.

"Mimi na Baba Levo tumezoeana sana, mara nyingi huwa anapoteza simu na simu yake inakuwa haina  vifurushi hivyo anataka kuingia Instagram aone, kwa hiyo nikimpa simu yangu huwa anaanza kukagua ili kujua nimempata nani au wakina nani wanatuma meseji za kutaka usajili mpya, bahati nzuri sina mambo mabaya kwenye simu yangu" ameeleza Shilole 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.