
Msanii Shilole 'Shishi Trump' .
Shilole ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Istragram baada ya kupokea barua kutoka kwa binti yake Rahma aliyopo katika shule ya Veritasn extended school akiwa anamshukuru kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi chote cha ukuwaji wake mpaka kufikia leo.
"Simkufuru Mungu kwa kuishi maisha ya shida niliyopitia, sisikitiki kwa kukosa elimu bora na kutotimiza ndoto zangu nyingi nilizokuwa nazo, nachojua mipango ya Mungu siyo kama ya binadamu", ameandika Shilole.
Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kufunguka kwa kusema "namshukuru Mungu kwa kila alichompa, jina, umaarufu, rizki, marafiki na ndugu wa kweli lakini zaidi watoto wangu ambao kila iitwapo leo ndiyo wananipa nguvu ya kuamka na kupambana, kuvumilia matusi, vikwazo na kila vipingamizi",
Licha ya Shilole kukosa elimu ya kutosha katika dunia ya sasa lakini hachoki kuwahimiza watoto wake wakazane katika masomo ili waje kutimiza ndoto zao walizojiwekea.