Jumamosi , 24th Jul , 2021

Presha ya mchezo wa watani wa jadi fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Yanga imezidi kuwa kubwa kwa pande zote mbili huku kila shabiki akitamba kwamba atamfunga mwenzake kwenye mchezo huo utakaochezwa Julai 25 Mkoani Kigoma.

Msanii wa filamu Bibi Mwenda kulia, kushoto ni mashabiki wa Simba

Kupitia EATV & EA Radio Digital, msanii wa filamu Bibi Mwenda ambaye ni shabiki wa Yanga amewatolea povu mashabiki wa Simba kwa kusema watapiga kwenye mshono kama walivyowafanya Julai 3 baada ya kuwafunga 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu.

"Nawahusia mashabiki wa Yanga Tanzania nzima kwamba tumewafunga hapa Dar es Salaam na tutawafunga tena Kigoma, tutawanunulia vitenge vya wax kubebea watoto wao, kama walienda kwa bus au ndege njia itawa-cost watapanda treni, Yanga oyeee" amesema Bibi Mwenda 

Zaidi mtazame hapo chini akizungumzia hilo