Alhamisi , 13th Aug , 2020

Hili ni fumbo ambalo amelisema msanii wa Taarab Mzee Yusuph baada ya kurudi tena kwenye muziki, ambapo alitangaza kuacha kufanya kazi hiyo miaka mitano iliyopita kisha kuhamia kwenye kuimba Qaswisda.

Mzee Yusuph

Mzee Yusuph amejibu hilo baada ya kudakwa na kamera za EATV & EA Radio Digital, ambapo ameulizwa kuhusu kuvunja ahadi yake aliyosema hatarudi kwenye muziki baada ya kutangaza kuacha na kilichosababisha kurudi kwenye Taarab.

"Watu walisema hawataki muziki kumbe wanataka sana, kwahiyo bado wanahaja na wanahitaji, pengo langu halijazibika na nafasi yangu ilikuwa kubwa sana kwenye huu muziki na hicho ndicho kilikuwa kimekosena na kupotea lakini sasa kimerudi, hakuna kiapo cha maskini kauli yangu ipo na itaendelea kuishi maamuzi yangu ni sahihi, mimi sio mtu mzima na sina ndevu za sineri" ameeleza Mzee Yusuph.

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.