''Sioni aibu, nilianza kutumia khanga'' Mimi Mars

Jumatatu , 3rd Jun , 2019

Msanii wa Bongofleva Mimi Mars amesema anajua changamoto za watoto wa kike wanapokuwa kwenye hedhi kisha kukosa taulo za kike (pads), kwani yeye mwenyewe amewahi kupitia wakati huo.

Mimi Mars

Akiongea na eNews ya East Africa Television, alipofika City Mall kutoa mchango wake kwenye kampeni ya Namthamini, Mimi aliweka wazi kuwa alianza kutumia khanga kabla ya pads hivyo anajua ni jinsi gani inamkosesha binti kujiamini.

Mbali na Mimi Mars, msanii Chemical naye amepongeza kampeni hiyo huku akishauri kuwa uwepo utaratibu wa wanafunzi kupewa pads shuleni kama ilivyo jeshini ambako yeye mwenyewe alijiunga na kukuta wanapewa bure.

Kwa upande wake Malkia Karen yeye amefunguka kuwa katika maisha ya sasa Pads zinahitajika sana ili kumfanya binti ajiamini muda wote akiwa na hedhi.

Wewe pia unaweza kuchangia kwa kuleta mchango wako kwenye ofisi za East Africa Television au kutuma kupitia akaunti no 0150431938200 CRDB jina Namthamini au Airtel Money namba 0787633313 jina East Africa Television.

Zaidi watazame hapo chini wakifunguka.