Alhamisi , 26th Aug , 2021

Hitmaker wa ngoma ya starehe Ferooz amewachana wasanii wa sasa wasiosapoti kazi za wakongwe kwa kusema wao ndio wana umaarufu wa ukweli kuliko wasanii ambao wanaupata Instagram.

Picha ya msanii Ferooz

Ferooz amefunguka kusema kibongobongo tayari ameshamaliza na hata umaarufu wao ni Original 'Og' na sio umaarufu wa Instagram 'IG' na followers wa wasanii wa sasa ambao Insta ikifa nao wanakufa.

Ferooz anasema wasanii wa sasa wanavimba kusapoti kazi za baadhi ya wasanii wa zamani kwa sababu ya kibiashara na wanawahofia wakiwapa sapoti watakuwa wanawapa nafasi.

Zaidi mtazame hapo chini kwenye video.