Ijumaa , 27th Aug , 2021

Mwimbaji wa muziki kutoka Kenya, Size 8 pamoja na mume wake Dj Mo wametangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto mwingine ambaye atakuwa wa tatu.

Picha ya Pamoja Msanii Size 8 na Dj Mo

Wote wawili wame-share picha kwenye mtandao wa instagram za kuonyesha ujauzito wa mtoto huyo ambaye wanamtarajia siku za hizi karibuni.

Mpaka sasa couple hiyo ina watoto wawili ambao ni Ladasha Belle Muraya ambaye alizaliwa Novemba 19, 2015 na Samuel Muraya Jnr naye alizaliwa tarehe 12 Novemba 2019.