Jumatatu , 2nd Jun , 2014

Msanii wa muziki wa injili, Solomon Mkubwa ameweza kung'ara huko Kenya baada ya kuibuka kama mshindi wa tuzo maarufu za Groove, kupitia kipengele cha msanii bora kutoka Afrika Mashariki na Kati.

Solomon akiimba jukwaani

Solomon katika tuzo hizi, amefanikiwa kuwapita wapinzani wake wakubwa akiwepo Rose Muhando na Christina Shusho kutoka Tanzania, Gaby Kwairize kutoka Rwanda, Exodus kutoka Uganda na David Kasika kutoka Congo.

Tuzo hizi kubwa zimefanyika huko nchini Kenya siku ya jana, zikiambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wakali kabisa wa muziki wa injili.