"Stereo is not my type" - Chemical

Friday , 17th Feb , 2017

Hatimaye kipindi cha eNewz cha EATV kimetegua kitendawili cha endapo rapa wawili wa Bongo Stereo na Chemical watakuwa wapenzi, baada ya Chemical kumvulia uvivu na kutamka 'LIVE' kuwa Stereo siyo wa aina yake, huku akieleza jinsi alivyomkera

Chemical na Stereo walipokutanishwa

Kupitia kipindi cha eNewz, Chemical amesema kuwa kwa uchunguzi alioufanya, amejiridhisha kuwa kila kitu alichokifanya Stereo ilikuwa ni 'drama' na kwamba hakutegemea kama Stereo angefikia hatua hiyo kwa kuwa alikuwa akimuheshimu kama kaka yake ambapo amesema jambo lililomkera zaidi ni njia aliyoitumia ya kwenye kwenye vyombo vya habari badala ya kumtafuta yeye mwenyewe.

Amesema ana uhakika Stereo hatafuti kiki kupitia yeye, lakini amemkaribisha kama anahitaji kufanya kolabo na yeye, yuko tayari kwa hilo. "Sidhani kama Stereo alikuwa anatafuta kiki kwangu, maana yeye ni msanii mkubwa, halafu alisema eti hafahamu pa kupata namba zangu, siyo kweli, alikuwa ana uwezo wa kuzipata sehemu yoyote" Amesema Chemical

Amesema baada ya mambo hayo yote, alimpigia simu na kumuuliza kama alikuwa 'serious' au lah, ambapo majibu aliyopata yalionesha kuwa stereo hakuwa 'serious', huku akiweka wazi pia kuwa jambo hilo limempa wakati mgumu kwenye familia yake na hata shuleni kuwa bado ni mwanafunzi.

Kwa upande wake Stereo amesema yeye alichokifanya ni kueleza ukweli wake kwa kuwa anamchukulia Chemical kama msichana mwingine, na siyo kama msanii.

Tazama majibizano yalivyokuwa katika kipindi cha eNewz.