Jumatatu , 29th Aug , 2016

Kundi la Clever Boys linaloshiriki hatua ya nusu fainali ya Dance100% limesema linafanya mazoezi kila siku kwa lengo la kuhakikisha linaibuka na ushindi wa mchuano mkali unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kundi la Clever Boys linaloshiriki Dance100%

Akizungumza na EATV Mwenyekiti wa kundi hilo Nicolas Martin amesema baada ya kufanikiwa kupenya hatua ya nusu fainali wanaendelea na mazoezi ya nguvu kuhakikisha wanalinda heshima yao kwa kuibuka washindi wa mwaka huu.

“Sisi mazoezi tunafanyia Chang’ombe TCC hivyo tunataka tulete heshima ndani ya jamii yetu huku tunakotoka pamoja na kuwaonyesha mashabiki wetu burudani ya aina yake” Amesema Nicolas

Ameongeza kuwa kitendo cha kujiunga na kundi hilo na kuweza kuwa pamoja kwa muda mrefu kumeweza kuwafanya kuishi kama ndugu na kusaidiana katika shida na raha.

“Sisi ni mara ya kwanza kushiriki Dance100% lakini tumeweza kuonesha umuhimu wa kuwa na kikundi kwa kushiriki Dance100% na mtaani kwetu tumeanza kujenga hamasa kwa vijana wengine” Amesema Nicolas

Shindano la Dance100% linarushwa na EATV pekee siku ya Jumapili kuanzia saa moja jioni chini ya udhamini wa Vodacom na Cocacola.

Tags: