Jumanne , 25th Feb , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, Tunda Man amewataka wasanii wa muziki nchini katika ngazi mbalimbali walizofikia, kurudi shule na kusoma muziki ili kuweza kufanyakazi hiyo kitaalam zaidi na pengine kujiongezea kipato katika sanaa wanayoifanya.

Tunda Man amesema haya kusisitizia mpango wake wa kuanzisha Shule ya Muziki ambayo itakuwa inafundisha wasanii namna ya kuimba kitaalam, ikiwa na madarasa yanayoongozwa na ma-professa mahiri wa muziki hapa Bongo, shule ambayo inatarajia kuanza huko Mbezi mwezi wa nne mwaka huu.

Tunda amesema kuwa, ni wakati sasa wa wasanii kuacha kubweteka na mafanikio kidogo waliyoyapata kimuziki na kuchukua hatua nyingine ya kusomea namna za kitaalam za kutumia sauti zao kuimba na hivyo kuongeza ubora katika kazi zao.