Jumamosi , 8th Aug , 2015

Usaili wa mwisho wa mashindano makubwa ya Dance 100% 2015, umetingisha anga leo katika viwanja vya Bascketball leaders Club Kinondoni, shughuli ambayo ilianza rasmi rasmi saa nne kamili asubuhi.

"Ubunifu katika mashindano", moja kati ya makundi yaliyojitokeza 'The Quest Crew' wakiwa wamevaa kininja.

Muamko na nguvu ya kutosha kutoka awamu ya kwanza na ya pili ya Usahili, vinaongeza chachu ya ushindani wa kutosha kuelekea kuwania nafasi chache zilizobakia za makundi ambayo yame na yale 10 ambayo tayari yameingia katika usahili.

Kumbuka hakuna kingilio, unaweza kufuatilia kwa karibu kila hatua ya mashindano hayo kuelekea kumpata mshindi kwa kufika mwenyewe kushuhudia, ni Dance 100% 2015.