Vanessa amefunguka kila kitu kwenye ukurasa wake wa instagram, baada ya kuandika ujumbe akisema anajua shughuli za mazishi ni kama ibada, hivyo hakuona haja ya kuweka wazi kuwa alihudhuria ama la, ingawa ukweli ni kwamba alikuwepo kwenye misiba hiyo.
Akiendelea kuelezea juu ya hilo, Vanessa Mdee amesema kwamba kutokana na kile alichokipitia baada ya kupoteza baba na dada yake, anajua uchungu wa kufiwa hivyo hakutaka kutumia matukio hayo kama jukwaa la kujionesha na yeye yupo.
Hivi karibuni Tanzania imekumbwa na misiba ya watu maarufu kwenye tasnia ya habari na burudani, ikiwemo msanii wa Hip Hop Godzilla, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde.