Jumatano , 24th Jan , 2018

Baada ya kufanikiwa kutoa na kuuza album yake ya kwanza inayoitwa 'Money Mondays', msanii Vanessa Mdee ameiambai eNEWZ kuwa mpenzi wake Jux pia anakuja na album yake.

''Jux ana album yake mpya ambayo mpaka sasa ameshamaliza kuirekodi anajipanga ili kuweza kuiachia hewani lakini mpaka sasa Jux amesharekodi Albam 5 ambazo zimekamilika tayari''. amesema.

Vanesssa amewaasa wasanii kuwa kelele zinazotolewa kwamba album haziuzi Bongo zisiwavunje moyo na kuacha kutoa album.Amesema kuwa yeye hakuvunjika moyo wakati anaanza kuandaa nyimbo zake za albam pamoja na watu kusema albam Bongo haziuzi yeye aliamini ni namna tu msanii ataandika nyimbo zake kwa ubora ili kukidhi mahitaji ya mashabiki. 

Vanessa kwa sasa yupo katika harakati ya kuuza albam yake ambayo anaiuza kwa njia ya mtandao na njia ya mkononi hivyo anawaomba mashabiki zake waweze kusapoti kazi yake ili waweze kukuza mziki wa Bongo. Fuatilia eNEWZ jioni ya leo kupitia EATV.