Jumatano , 5th Oct , 2022

Staa na mfanyabiashara aliyekuwa anatishia kwa shepu yake Afrika Mashariki Vera Sidika kutoka Kenya, amefanya upasuaji wa kupunguza muonekano wa makalio yake kwa sababu matatizo ya afya.

Pichani hapo ni muonekano wake wa zamani na muonekano wake mpya

"Kuzaliwa upya, Hii imekuwa awamu ngumu zaidi maishani mwangu kwa sababu ya hatari na matatizo ya kiafya , ilinibidi kufanyiwa upasuaji. Nimekubali na nimejifunza kujipenda bila kujali".

"Nitakuwa nikiweka video zangu za safari ya upasuaji hapa, kwa wale ambao wamekuwa wakifikiria kupata upasuaji wa nyara au kubadilisha chochote kwenye miili yao hii inaweza kubadilisha mawazo yako". Ujumbe wa Vera Sidika baada ya kufanya upasuaji.