Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

VIDEO: Wema aeleza sababu ya kukimbilia CHADEMA

Ijumaa , 24th Feb , 2017

Msanii wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) siku moja moja baada ya taarifa hizo kusambaa kupitia mitandao ya kijamii.

Wema sepetu akizungumza na wanahabari

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.

Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana, kwa sasa I am a proud member of CHADEMA". Amesema Wema Sepetu

Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.

"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike"  Amesema Wema

Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu

Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM kusema "Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki

Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia" 

Tazama hapa video kamili ya tukio lenyewe..

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali