Jumamosi , 16th Aug , 2014

Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na EATV, leo hii imeanza zoezi la kutembelea washiriki wa shindano ya Dance 100% 2014 katika kambi zao za mazoezi ili kuangalia mchakato wa maandalizi ya makundi haya kuelekea hatua ya robo fainali.

Meneja Mahusiano Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiwa (katikati mwenye T-Shirt nyeusi) na kundi la Mazabe Powder katika kambi yao Tegeta Dar es Salaam leo.

Zoezi hili limeanzia huko Tegeta jijini Dar es Salaam, ambapo leo timu hii imekutana na kundi la Mazabe Powder na kujionea jinsi maandalizi yao yanavyokwenda.

eNewz ambayo imefuatilia zoezi hili kwa karibu, imeweza kuongea na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bwana Matina Nkurlu ambaye amesema kuwa zoezi hili ni kwa ajili ya kuwahamasisha washiriki kuitumia nafasi hii kwa nguvu na nia moja ikiwa kama fursa ya ajira pia, na kuwahakikishia kuwa Vodacom ipo nao bega kwa bega.

Vilevile muwakilishi wa kundi la Mazabe Powder, Francis Charles ama Dogo JJ akazungumza na kutoa shukrani zake kwa Vodacom na EATV kwa nafasi hii na kuweka wazi kuwa wamewekeza jitihada za kutosha kuleta ushindani mkubwa katika mashindano haya mwaka huu.

Zoezi hili litaendelea tena siku ya kesho kuyafikia makundi mengine yanayoshiriki Dance 100% 2014 katika kambi zao.