"Waendelee kulala,hatutaomba lifti"-Country Boy

Jumatano , 15th Jan , 2020

Rapa Country Boy amewachana wasanii ambao wanaogopa kuachia Album, na kusema waache waendelee kulala, huku yeye akiendelea kufanya kazi.

Pichani ni msanii wa HipHop Country Boy

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, wakati wa uzinduzi wa Album yake aliyoipa jina la Yule Boy, amesema namba za mauzo hazidanganyi kwa sababu, Album yake inafanya vizuri na inazidi kupanda kila siku.

"Namba hazidanganyi kila siku namba zinaongezeka, kwangu mimi naona ni baraka kwenye mwezi mmoja kupitia mauzo ya mitandaoni nimeuza Milioni moja na laki mbili au laki tatu, pia nina ngoma nyingi za Kimataifa ambazo zinakuja kama Seyi Shay kutokea Nigeria, na msanii mmoja mwenye rasta kutokea Marekani ila jina simtaji" amesema Country Boy.

Aidha akizungumzia juu ya wasanii wengine kuogopa kuachia Album kwa sababu wanaogopa kama hazitauza sokoni, Country Boy amewachana kwa kusema.

"Waendelee kulala sisi tunaendelea kufanya kazi, wakiamka watatukuta sisi tushafika mbali hatutaomba lifti kipindi ambacho watabidi wakodi uber kutufuata tulipo".