Jumatatu , 30th Nov , 2020

Muigizaji Prince HDV amekana madai ya kulelewa na mwanamke kwa kusema wamama wengi wa mjini wana moyo wa kutoa vitu vyao kuwapa vijana ambao wamebarikiwa vipaji ndiyo maana akipewa hawezi kukataa.

Katikati ni muigizaji Prince HDV

Akifunguka zaidi kuhusiana na hilo Prince HDV ambaye amepata umaarufu mkubwa wa kuigiza kama kiben-ten kwenye tamthilia anazocheza amesema kuwa 

"Kuna wakati mwanamke anatokea anakupa mwenyewe hauwezi kukataa ila sio kwamba nalelewa halafu wamama wengi sana wa mjini wana moyo wa kutoa kwa vijana ambao tumebarikiwa vipaji ila hatuna kitu na wanatusaidia sana kwenye maisha yetu ya kawaida, na kwenye kupewa huwezi kupata bure lazima ujitume" amesema Prince HDV 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video