
Nikki Mbishi (kushoto) na Nash MC (kulia)
Desemba 31 kuelekea mkesha wa mwaka mpya, katika mtandao wa Twitter, Nikki Mbishi alianzisha mjadala mzito juu ya elimu ya Nikki wa Pili, akihoji kitendo cha watu kumwita 'Msomi'.
"Hili suala la Nikki wa Pili "msomi" nani aliliidhinisha liwe nyeti hivyo, mbona hata hoja zake ni za bei chee tu. Muda mwingine kama watu wengine hawaeleweki?. Mbona Mwana FA ana Masters Degree kabatini na kauchuna tu, au ni vile presenters wengi ni tabu darasa ndio maana wanaona ajabu?," ameandika Nikki Mbishi.
Nash MC ambaye pia ni msanii wa Hip Hop nchini naye akachangia mjadala huo, pale alipoandika, "Hahahahahahahahahahahaha mimi nimesoma lakini sikusomea kuwa kibaraka na kujipendekeza".
Baada ya kuanzisha mjadala huo, wadau mbalimbali walijitokeza na kutoa maoni yao juu ya kauli hiyo ya Nikki Mbishi. Wachache kati ya waliochangia ni mtumiaji aliyejulikana kwa jina la Frank Daxx ambaye ameandika, "kwani ni tatizo kujiita msomi?. Elimu inaongea sio mbaya".
Mwingine ambaye anajulikana kwa jina la Mommentum Producer amechangia kwa kuandika, "ingekua vizuri zaidi kama kwenye mfano wako ungejiweka wewe mwenyewe. Ila kwa vile hujajiweka wewe, hoja yako ndio ya bei chee sana. Acha tu Nikki wa Pili aendelee kuwa 'MSOMI'".