"Wanyakyusa ndivyo tulivyo" - Amber Lulu

Jumatatu , 22nd Jun , 2020

Msanii Amber Lulu amefunguka na kusema kabila la Wanyakyusa lilivyo kila mtu huwa ana matatizo yake ila yeye binafsi hanaga noma na mtu yeyote.

Msanii Amber Lulu

Hilo limekuja baada ya kuulizwa kuhusu uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kati yake na rafiki yake Gigy Money, ambaye kuna muda wanakuwa wapo sawa na kuna muda wanakuwa na utofauti.

"Hilo suala nilishalifikiriaga ikitokea kukiwa na uhitaji tutafanya, Wanyakyusa ndivyo tulivyo kila mtu anakuwa na matatizo yake, mimi sinaga noma wala muda huo ila akipiga kushoto mimi napiga kulia, akinicheki pia poa yaani fresh tu" amesema Amber Lulu.

Tazama mahojiano kamili hapa chini