Jumatatu , 11th Jan , 2016

Mwimbaji maarufu wa miondoko ya Taarab Omar Tego kutoka kundi maarufu la miondoko hiyo ya taaraba la Coast Modern Taarab, ameamua kuwekeza nguvu zaidi kwa kuibua kikundi cha vipaji vya watoto wao ambao wanajulikana kwa jina la Vijukuu wa Teggo.

Mwimbaji wa Taarab Omar Teggo akiwa na kikundi chake cha 'Vijukuu wa Teggo'

Watoto hao ambao waimbaji wake ni Tarik, mtoto wa Maua Tego na Khairat ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Omar Tego, wameweza kuwateka mashabiki kwa uwezo wao wa kuimba wakiwa bado wangali wadogo kwa kutoa wimbo wao mpya uliobatizwa jina 'Mama wa Kambo'.

Omar Tego ambaye ni msanii maarufu wa muziki nchini ameongea na eNewz akielezea kuwa huu ni wakati wa kuwatambulisha zaidi vijana wake akiwandaa ili waweze kujiendeleza na vipaji vyao katika sekta ya muziki.