
Picha ya hali ya jua
Akizungumza hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Rehema Bombo amesema sasa hivi kila mtu anaelewa changamoto kubwa ya dunia kwenye mabadiliko ya tabia nchi na lengo lilikuwa ni ku-manage 'temperature' iweze kushuka mpaka 1.5
"Serikali wadau mbalimbali Afrika na duniani kote suala 'climate change' analihisi kila mtu na watu wa hali ya chini ndiyo wanapata madhara zaidi kwa sababu mtu wa hali ya chini anatagemea akalime shambani sasa jua linavyowaka hivi na joto lilivyo juu" amesema Rehema Bombo
"Pia mtu wa hali ya chini mtoto wake ndiyo anatembea kwa miguu kwenye jua la saa 7, 8 au 9 akiwa anatoka shule, mwenye maisha mazuri ana gari lake lina AC au hata nyumbani kwake kuna AC"
Aidha Mwanaharakati huyo amemaliza kwa kusema "Kama hatutachukua hatua ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi maisha sijui yatakuaje maana hali ni ngumu, sasa hivi watu hawana stress za umaskini wala njaa lakini hali ya hewa inatupa stress kubwa"