Wema afungukia uhusiano wake na Diana

Jumatano , 10th Apr , 2019

Mwanadada asiyeishiwa matukio kutoka kiwanda cha Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa yeye atabaki kuwa dada wa msanii mwenzake Diana Kimaro na si vinginevyo.

Wema Sepetu akiwa na Diana.

Wema amesema kuwa atasimama kama dada kama anavyofanya kwa wadogo zake wengine katika tasnia na nje ya tasnia na ameshapunguza baadhi ya marafiki wasiofaa.

"Mimi nitabaki kuwa dada kwa Diana kama nilivyo kwa Allu au Lulu, wote wale wadogo zangu hakuna kingine", amesema Wema.

Akizungumzia uhusiano wake na mama yake amesema kuwa, mama yake kukasirika ni kawaida na kama mama akichukizwa na mwanaye anatakiwa kuwa hivyo lakini wako sawa.

Hayo yanajiri baada ya mama mzazi wa mwanadada huyo kumzuia urafiki na muigizaji mwenzake Diana Kimaro kwakile alichodai kuwa urafiki wao hauna faida.