Whozu ajibu kuhusu kufanya mapenzi kwenye gari

Ijumaa , 12th Jul , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania Whozu "Dingoo", amefunguka kuwa ameshawahi kuazima magari ila hajawahi kufanya mapenzi kwenye gari.

Whozu

Whozu amesema hayo wakati alipofanya mahojiano na EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa suala la yeye kuazima gari pamoja na swali la kizushi kama aliwahi kufanya mapenzi kwenye gari haswa baada ya kutamba sana baada kununua gari yake.

"Huo utoto wa kufanya mapenzi kwenye gari sijawahi kufanya, nilishaazima gari kitambo, niliazima tu kwa michongo ya hapa na pale kipindi ambacho sina gari, lakini kwa sasa hivi Mungu kanijaalia uwezo wa kuwa na gari yangu, kuwa na maisha yangu, muziki wangu na mashabiki zangu wananipokea".

Pia Whozu amefunguka kuhusu kauli ya Dogo Janja ambaye aliwahi kusema wasanii wapya hakuna na waliopo wanapungua kwa kusema, ''Janjaro ni mtu wa utani sana, ni mtu ambaye anaandika caption nzuri lakini sio kila muda yupo seriazi sana''.