Ijumaa , 6th Dec , 2019

Muigizaji na mbunifu wa mavazi, Jacqueline Wolper, amesema huenda akawa na upepo mzuri, ambao unawafanya wanaume anaokuwa nao kwenye mahusiano kuwa maarufu.

Muigizaji wa Filamu, Jacqueline Wolper.

Wolper amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, wakati alipowasili kwenye sherehe ya kula mlo wa jioni kati ya wasanii wa filamu na waandishi wa habari.

"Hapana, labda tu ninakuwa na upepo nao lakini hata wangekuwa na watu wengine, kwa kazi ambazo wanazozifanya na jitihada walizonazo wangekuwa tu mastaa, msilete maneno kwamba mtu fulani amemfanya mwingine kuwa staa" amesema Jacqueline Wolper. 

Aidha Wolper ameendelea kusema mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, hayajamuathiri kivyovyote licha ya kuondoka sehemu aliyokuwa akifanyia kazi na kujitegemea mwenyewe.