Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Amber Lulu amesema wakati yupo kwenye mahusiano na msanii huyo alimfanyia tukio lililomuumiza zaidi, baada ya kugundua kampikia chakula na kumpelekea, ili ale na mwanamke mwengine.
“Nakumbuka D alinipigia simu akaniambia nimetoka studio, akaniambia nipikie kile chakula ninachokipenda halafu niletee hoteli, alikuwa hoteli mi nikajua labda amechoka kwenda nyumbani baada ya uchovu wa studio, nikajipikilisha nikawa nampelekea, nilivyopeleka nikakutana na msichana kwenye mlango wa pili, lakini mazingira yalikuwa hayanishwishi”, amesema Ambaer Lulu.
“Nikatoka nje nikakutana na muhudumu wa mapokezi, nikamdanganya huyu ni ndugu yangu na hajaonekana nyumbani tangu jana, alikuwa na nani na mbona anaonekana amechoka hivi, muhudumu akaniambia kuwa alikuwa na Young D na wana siku ya pili pale, kumbe alikuwa mwanamke wake kama mke nakwambia, niliumia sana, nikaondoka zangu”, aliendelea Amber Lulu akisimulia tukio hilo.
Akizidi kutupa michapo ya kilichotokea siku hiyo, Amber Lulu amesema kuwa kitu ambacho kilimuuma zaidi ni kwamba alikubali kujinyima kwani kwa siku hiyo hakuwa na pesa kabisa, lakini alikubali kupika ili mpenzi wake huyo akale.
“Yaani ile siku sikuwa na hela kabisa, na kadi yangu ya benki ilimezwa, kwa hiyo kihela ambacho nilikuwa nacho nikajinyima nikapika mtoto wa watu nimpelekee tule, naenda kule ndo hayo niliyoyakuta aisee niliingia studio nikawa naimba huku nalia”, amesema Amber Lulu.
Wawili hao kwa sasa wameshaachana, lakini amekiri kuwa bado ana hisia za kimapenzi kwa Young D.

