Jumanne , 26th Nov , 2019

EATV & EA Radio Digital imepiga stori na rapa Young Dee, ambaye ameweka wazi kuwa Mama yake hapandi tena daladala baada ya kumnunulia gari, pia sasa hivi anatumia muda mwingi kukaa na mwanae tofauti na zamani ambapo alikuwa anatumia kuwa na washkaji.

Msanii Young Dee akiwa na mama yake mzazi kwenye gari

Young Dee ambaye amerudi nchini Tanzania, baada ya kukaa Marekani kwa muda wa miezi 6 amesema, mama yake amehangaika sana ila sasa hivi hapandi tena daladala.

"Mama yangu yupo sawa sasa hivi, amepanda sana daladala, siwezi kusema ni gari la aina gani na shilingi ngapi ndiyo maana nashangaa hata hizo stori mmezipatia wapi, ila jueni tu Mama yangu sasa hivi ana usafiri na haishi tena yale maisha ya kugombania daladala" amesema Young Dee.

Aidha Young Dee akizungumzia suala la malezi ya mwanaye amesema, yupo katika uangalizi wake na Mama yake ila hataki kumhusisha na mitandao ya kijamii.

"Mwanangu yupo poa pia yupo katika uangalizi wangu na Mama yangu, zamani nilikuwa na muda mwingi wa kuzunguka na washkaji ila sasa hivi muda mwingi nakuwa na mwanangu, ila sipendi kumpeleka katika mitandao kwa sababu sijui atapenda mambo ya mitandao endapo atakapokuwa mkubwa" ameongeza.