
Picha msanii Young Lunya (kushoto) na Joh Makini (kulia)
Kupitia ukurasa wa instagram YL ambaye yupo chini ya usimamizi wa Intersource Records ame-share picha akiwa na mwamba wa kaskazini Joh Makini na kuacha ujumbe usemao “kuna ngoma moja nimeshirikiana na Joh Makini kwenye Abum yangu”.
Picha ya pamoja msanii Young Lunya (aliyesimama) na Joh Makini (aliyekaa) wakiwa ufukweni.
Hii itakuwa sio wimbo wa kwanza kwa wawili hawa kufanya pamoja kwani Joh pia aliwahi mshirikisha kwenye ‘Mchele’ mwaka mmoja uliopita.