
Msanii Z Anto na Binti Kiziwi
Z Anto amesema Binti Kiziwi alikuwa hawezi kusimama mbele ya jamii, aliigopa Serikali na baadhi ya watu pia alikuwa hataki kuonekana kama amerudi baada ya kutoka gerezani kwa sababu alihofia kuingia tena kwenye matatizo.
"Nilikuwa na lengo la kumtengenezea mtaji ili kupambana na maisha yake, wakati nawaza kumsaidia akapata wengine wakamshauri na kumshawishi mwisho wa siku nikaishia hapo, kwa asilimia nyingi alinufaika na mimi kwa sababu alikuwa hawezi kusimama mbele ya jamii, aliiogopa Serikali na baadhi ya watu, nilikuwa naye na nilimtambulisha tena kwa jamii ili aonyeshe kitu anachotaka kukifanya" ameeleza Z Anto
Binti Kiziwi na Z Anto waliwahi kuwa kwenye mahusiano kipindi cha nyuma baada ya kumaliza kufanya kazi ya pamoja kwenye video ya wimbo wa 'binti kiziwi' ambayo ilitoka mwaka 2008.