Zari atoboa siri ya kupendeza kwake

Jumatatu , 13th Mei , 2019

Mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Uganda ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari’ amekiri kuwa kuvaa nguo zinazoitwa feki huku akiweka wazi kwamba anachoangalia yeye ni kupendeza kwake.

Zarina Hassan.

Zari ametoa kauli hiyo alipoulizwa kwamba anavaa nguo za gharama za kiasi gani, ambapo amesema yeye huwa anavaa nguo yoyote, haijalishi ni ya gharama kiasi gani isipokuwa tu iwe inampendeza mwilini. 

Unajua mimi siwezi kukuambia kuwa ninavaa nguo za gharama flani ya juu, hapana, hata nguo za Kariakoo mimi navaa tu ilimradi ikikaa kwenye mwili wangu inanipendeza, si nguo tu hata nywele mimi navaa yoyote ile ili mradi nipo smati", amesema Zari ambaye alionekana kuwajibu watu waliokuwa wakidai kuwa anavaa nguo feki za Kichina ambazo zimejaa Kariakoo.

Mwanadada huyo alikuja nchini wiki iliyopita kikazi na kulakiwa na mashabiki wengi ambao ndio wanamsapoti.