Ageuka mchungaji baada ya kusomewa mashtaka

Jumamosi , 8th Jun , 2019

Mwanaume mmoja ambaye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kuiba kitabu cha hundi (cheque) chenye thamani ya shilingi mia mbili na kukitumia kujipatia sh 880,00 za Kenya, ambazo ni zaidi ya milioni 19 za Tanzania kutoka Benki ya Equity, aliushangaza umma

baada ya kigeuza mahakama hiyo kuwa sehemu ya mahubiri.

Mwanaume huyo ambaye alijulikana kwa jina la Steve Gordon Ochieng, amesema kwamba yeye ni mchungaji na kwamba shetani ametumiwa kuharibu huduma, lakini kamwe hatafanikiwa kwani yupo kwenye matengenezo ya kutumiwa na Mungu.

“Mimi ni mchungaji, nguvu za shetani zimeungana kuangusha na kuharibu huduma yangu kabisa, hawatafanikiwa kwa jina la Yesu, kila mmoja ndani ya mahakama hii anatakiwa kuacha dhambi na kutubu, kuutafuta uso wa Mungu na kupata wokovu”, alisikika Mr. Ochieng akihubir mahakamani hapo huku akiwa kizimbani.

Bw. Ochieng ameendelea kwa kusema kwamba licha ya nguvu za kishetani na mkuu wao, wamekusudia kuingilia wito wake.