Alichosema Piere Likwidi baada ya kutoka Karantini

Jumanne , 5th Mei , 2020

Mchekeshaji Piere Likwidi amesema, sasa hivi amepona ugonjwa wa Corona baada ya kuruhusiwa kutoka Karantini kwenye Hospitali ya Amana, wiki iliyopita ambapo alikaa kwa siku 14.

Mchekeshaji Piere Likwidi

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, kuhusu maendeleo yake, maisha ya Karantini na alichojifunza kuhusu ugonjwa wa Corona Piere Likwidi amesema,

"Nimepona kabisa nina kama wiki moja nanusu nimetoka Karantini, nilikuwa nafanya sana mazoezi Karantini ndiyo yamenisaidia hukywu nakuna maji ya machungwa, malimao na tangawizi, wote nilioingia nao hali zetu zilikuwa sio nzuri ila sasa hivi tunaendelea vizuri" amesema Piere Likwidi.

"Huu ugonjwa ni kama magonjwa mengine na unapita tu uwezekano wa kupona upo, watu wasiwe kwenye hofu kwamba wakiumwa hawawezi upona au watakufa, ukiona dalili bora uende hospitali maana ndiyo itakuwa nafuu yako" ameongeza.