Baada ya TID, Blue na Harmonize sasa zamu ya Wema

Jumanne , 12th Mei , 2020

Staa wa filamu na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, amesema endapo Corona ikiisha na utalii wa ndani ukianza, atataka aitwe jina la mnyama Twiga huku akilikataa jina la Nyumbu.

Mrembo na msanii wa filamu Wema Sepetu

Wema Sepetu ametangaza hivyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika  "Tanzania kuna mbuga za wanyama halafu kuna wanyama binadamu, Corona ikiisha tukianza Utalii wa ndani, mtakapomuona Twiga mumuite Wema, huyu ndiyo mnyama nafanana naye, mambo yenu ya kuniita Nyumbu mnikome jamani mimi naenda kama Twiga"

"Kwanza nimekaa ki Twiga Twiga kabisa Nyumbu sitaki, pia nilikuwa nalizimia lakini tatizo linakuja kwenye mfanano, i am not Nyumbu i am Twiga, Wema the Tz sweetheart, Wema the giraffe, Wema the last born vinaenda ila Wema the Nyumbu mmmmmh sijui ila sina uhakika saaana ila fresh tu, kwani kitu gani" ameongeza.

Kwa hiyo Wema Sepetu anaungana na wasanii kama TID, Mr Blue, Harmonize, Afande Sele, Country Boy, Young Lunya na Isha Mashauzi kama wasanii ambao wanajiita majina ya wanyama.