Jumanne , 10th Sep , 2019

Siku moja baada ya Mbunge wa Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla kuweka wazi kuwa amejiondoa kwenye chama cha Mabaharia, sasa ametangaza kurejea.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kigwangalla ameeleza kuwa amepitia vizuri kanuni na miongozo ya chama hicho, na kugundua kuwa hazimpi nafasi ya kujiondoa.

''Ubaharia mtu hajiungi ukubwani, ni jambo la asili, unazaliwa nao! Huwezi kujitoa, wala baharia hazeeki. Baharia haachi wala hatolewi. Once a baharia always a baharia. Hivyo wazee wameniasa kwamba kwa ukongwe wangu, siwezi kujitoa maana sikujiunga, nabaki kuwa ‘baharia emeritus!’', ameandika.

Ikumbukwe kuwa Baharia ni Usemi ambao kwa sasa umekuwa ukitumika na watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, ukimaanisha wanaume ambao wakisaidiana mara kwa mara, hasa kwenye masuala mbalimbali ikiwemo familia au kuunga mkono jambo wanaloamini wao.

Kwa mujibu wa Kamusi Sanifu, neno Baharia maana yake ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha usafiri majini, hasa baharini kama vile boti, mashua, jahazi au meli. "Mwanamaji" hutumiwa mara nyingi kwa kutaja mabaharia wa kijeshi.

Tweet ya Kigwangalla imekuja muda mfupi baada ya Tinga namba moja kwa vijana East Africa Television, kurudi kibaharia kwenye King'amuzi cha Azam TV, kupitia Channel namba 118, na sasa unaweza kutazama burudani zote.